WANAWAKE MSICHELEWE KUZAA, KUEPUKA MATATIZO YA AFYA YA UZAZI

0 comments
https://www.facebook.com/theclicktz
Wanawake wanaochelewa kuzaa wanakabiliwa na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio utafititi tu balo maoni ya daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya.
Athari za kuchelewa huko ni pamoja na kukumbwa na utasa, tisho la kupata Saratani ya kizazi na matiti pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.
Wanawake wengi wanaofanya kazi huchelewa kuzaa mtoto wao wa kwanza hadi wanapofika umri a miaka 35 badala ya kuzaa wakiwa na umri wa miaka 24-28.
Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya afya ya uzazi.
Mtaalamu wa afya ya uzazi mjini Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu hoja hii alinukuliwa akisema kuwa ''wanawake kwanza wanataka kusoma masomo ambayo hayaishi, daima wako madarasani na ofisini na kuahirisha kuzaa mtoto wao wa kwanza hii ni hatari kubwa.''
Bwana Ong'ech alisema kuwa wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au uvimbe katika kizazi, na hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi au HIV.

Fibroids zinasababishwa na kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya kupanga uzazi kwa mda mrefu.
Wanaochelewa kuzaa pia wanakabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .
Hatari hizi ni nyingi tu, sasa chaguo ni kwako.

Soma Zaidi »

MATUNDA NA MBOGA MBOGA VINAWEZA KUOKOA MAISHA: SOMA ZAIDI

0 comments
https://www.facebook.com/theclicktz
Watafiti nchini Uingereza wanasema kula matunda na mboga za majani mara saba kwa siku inakuwezesha kuwa na afya zaidi kuliko mara tano iliyokuwa imependekezwa hapo awali na shirika la afya duniani
Utafiti huu mpya unasema kuwa kula matunda mara saba kwa siku kunaweza kuokoa maisha yako kutokana na vifo vya mapema.
Utafiti uliofanyiwa wanaume na wanawake, 65,226, ulionyesha kuwa matunda mengi aliyokula mtu mmoja yalimpunguzia uwezo wa kufariki katika umri wowote.
Eti wanasema kuwa ikiwa utakula matunda mara saba kwa wiki uwezo wako wa kupatwa na magonjwa yanayotishia maisha yako, unapungua kwa asilimia 42.
Wataalamu wanasema kuwa mifumo mingine ya maisha kama vile kutovuta sigara na kutokunywa pombe kupindukia pia imechangia kupungua kwa vifo.
Wanasema kuwa hawakuzingatia tu faida za Matunda na mboga bali mambo mengine mengi.
https://www.facebook.com/theclicktz
Watafiti katika Chuo kikuu cha University College London, walitathmini Data iliyokusanywa kati ya mwaka 2001 na 2008, iliyowapa mweleko kuhusu afya ya watu wanaokula matunda kwa wingi.
Utafiti huo ulitathmini idadi ya vifo kwa ujumla pamoja na vifo vinavyotokana na Saratani, maradhi ya Moyo na Kiharusi na kugundua kuwa vifo vya mapema vilipungua kulingana na mtu anavyokula matunda na mboga za majani.
Mboga za majani ndizo zilikuwa na uwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi hjata zaidi ya matunda.
Maji ya matunda hayakuwa na manufaa makubwa huku matunda yanayopakiwa kwenye mikebe yakionekana kuongeza tisho la kifo.
Wataalamu wanasema kuwa wangali wanaendelea na utafiti wao na kwamba kuna mambo mengine mengi yanayochangia afya ya mtu.
-BBC

Soma Zaidi »

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI HUKO MBEYA YA TEKETEA KWA MOTO

0 comments
https://www.facebook.com/theclicktz
Mabweni ya shule ya sekondari ya Ivumwe Mbeya yenye mchepuko wa Wavulana na Wasichana yateketea kwa moto!

Soma Zaidi »

JARIDA MAARUFU LA PEOPLE NCHINI MAREKANI LIMEMTANGAZA MKENYA LUPITA NYONG'O KAMA MWANAMKE MREMBO ZAIDI DUNIANI MWAKA 2014

0 comments
https://www.facebook.com/theclicktz
Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu '12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki hii ya jarida hilo.

Jarida la People limemtaja Lupita kuwa mwanamke mrembo
Stacy Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.

Hatua ya Jarida la People ambalo huchapishwa kila wiki nchini Marekani na kusomwa na karibu watu milioni 40, kumkubali Lupita kama mwanamke mrembo duniani, ni kama tuzo kivyake kwa muigizaji huyo ambaye amegonga vichwa vya habari nchini Marekani tangu kushinda
Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.
"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufiia chochote maishani mwao.
-BBC

Soma Zaidi »

WATU WA NNE WAUAWA KATIKA MLIPUKO MWENGINE NAIROBI

0 comments
https://www.facebook.com/theclicktz
Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.
Bomu la pili lilipatikana katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao ambayo iliharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.
Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi.
Bosco Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la kuingia kwenye kituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.
Alunukuliwa akisema:"kile kilichonikuta katika kibanda changu ni nyama ya watu iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje."
Mtaalamu wa maswala ya usalama jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo lililipuka baadaye.

Soma Zaidi »

UTAJIRI WA IRENE UWOYA WAANZA KUWA GUMZO, WATU WAHOJI AMEPATA WAPI MALI ZOTE HIZO

0 comments
https://www.facebook.com/theclicktz
Inadaiwa kuwa hali ya hewa imechafuka kwa msanii nyota wa filamu za Bongo Irene Uwoya ambapo ameshindwa kutaja vyanzo vya utajiri wake wa Ghafla, Hivi karibuni Uwoya alikaririwa akisema kuwa hawezi kutaja kazi nyingine anayofanya na utajiri aliokuwa nao kwani wapo baadhi ya watu hawapendi kuona mmoja wao akiendelea ...Alisema kuwa pamoja na magari anayomiliki ya kifahari hawezi sema ni njia gani amepata utajiri huo..Nimefanya Filamu kadhaa ambazo zimenipa hela na cha zaidi ni Jina ambalo limenifanya kupata Deals zingine zinazonipa Pesa..Jina langu ni Kubwa so lazima liendane na Mali ninazopata..alisema uwoya

Soma Zaidi »

Waswahili wanasema "KILA AJALI MWANZO WAKE NI MAKUSUDI

0 comments
https://www.facebook.com/theclicktz
Duniani vituko haviishi. Kila siku jipya haya wadau nisaidie nani hayuko sawa hapa ndugu ngo'mbe au ndugu mtu

Soma Zaidi »
Copyright © 2013. Theclicktz - All Rights Reserved